Hi!! Natumai uko poa. Kama kawaida leo napenda nikujulishe kuhusu simu nyingine ambayo bado iko sokoni na rasmi imezinduliwa mwezi wa nane mwaka 2016.Simu hii si nyingine ila ni kutoka kampuni ya Tecno simu iitwayo Tecno C7.
Kumbuka kampuni hii ilishatoa matoleo mengine ya C kama vile C8 na C5 ambazo kiukweli zilifanya vizuri sana sokoni hasa kupitia uwezo wao mkubwa wa kuwa na camera nzuri.
Simu hii ya Tecno C7 ina uwezo wa kutumia internet kwenye mitandao ya 2g,3g na mtandao wa kisasa wenye nguvu zaidi hapoa nchini kwetu wa 4g.N hiyo ikiwa na maana kuwa unapokuwa na simu hii huna haja ya kuwaza kuhusu spidi ya internet yako kwenye simu hii kwani utaweza kudownload files za aina mbali mbali na zenye ukubwa mkubwa kwa muda wa dakika tu au sekunde.
Simu hii ukubwa wake wa nafasi ya kuweza kuhifadhi vitu mbali mbali kama music,programu na files nyingine nyingi yaani internal storage yake ni ukubwa wa 16 GB,na hivyo kukufanya kutokuwaza kuhusu simu yako kuwa na nafasi ndogo.Kizuri zaidi ni kwamba pamoja na simu hiyo kuwa na nafasi hiyo kubwa ya kuhifadhi vtu pia simu hiyo ina sehemu nyingine ambayo unaweza kuweka memory kadi yako nyingine ya ukubwa wowote na hivyo kufuta kabisa swala la kuishiwa nafsi kwenye simu yako.Lakini kizuri zaidi na kikubwa pia kwenye simu hii ni kwamba simu hii ina RAM ya 2GB,Ram hii inakuwezesha wewe kufungua programu nyingi kwenye simu yako hii kwa wakati mmoja na ukazitumia kwa wakati mmoja bila simu kukusumbua kuwa nzito wala kukwama kwama na kwa uhakika simu yako hii itakuwa na spidi kubwa sana hata katika kufungua vitu mbali mbali ndani yake.Lakini pia RAM hii itakufanya uweze kucheza games zenye ubora wa hali juu na zenye ukubwa mkubwa bila kukwama kwamba kwenye simu yako hii,ama kwa hakika utacheza kwa raha kabisa tena ikiwa na spidi ya uhakika.
Simu hii ina ukubwa wa nchi tano (5) na hivyo si haba kwani utaweza kuitumia bila kukonyeza macho yako na pia ikiwa na kioo ambacho kina ng'aa vizuri kabisa.Kma kawaida Tecno wameamua kufanya kweli kuhusu kamera kwani simu hii ina uwezo wa kupiga picha bora kabisa iwe unatumia kamera ya mbele au ya nyuma picha zake ni bora sana na hivyo kukufanya usipitwe na tukio kwani utaweza kupiga picha ambazo kwa hakika kila mtu atazipenda.
Kamera ya simu hii ama kwa hakika ni moto wa kuotea mbali kwani kamera ya nyuma ina 13MP hali kadhalika ya mbele nayo ina 13MP.bila kusahau ina uwezo wa kuflash katika kamera hizo zote mbili.Simu hii hutajuta kuwa nayo.
Mengine kuhusu simu hii tazama hapa chini ila kwa hakika simu hii ni bora kabisa na isikupite mjanja.
General Information
2G Network | GSM 850 / 900 / 1800 / 1900 |
3G Network | HSPDA 850 / 2100 |
4G Network | LTE |
SIM | Dual mini SIM |
Status | Available August 2016 |
Body |
|
Dimensions | 142.1 x 71 x 5.4 mm |
Keyboard | Touchscreen |
Colors | Black, Gold |
Cover | Plastic |
Display |
|
Type | IPS capacitive touchscreen with 16,000,000 colors |
Size | 5.0 inches, 720 x 1280 pixels, 294 pixels per inch (PPI) |
Memory And OS |
|
Card slot | MicroSD card, up to 128GB |
Internal | 16GB |
OS | Android 6.0 Marshmallow |
Processors | 1.3GHz quad-core Cortex-A53 CPU, MediaTek MT6735 chipset, Mali-T720 GPU |
RAM | 2GB |
Audio |
|
Alert types | Vibration, MP3 ringtones |
Loudspeaker | Yes |
Audio port | 3.5mm jack |
Connectivity |
|
2G | GPRS – up to 85.6 kbps; EDGE – up to 236.8 kbps |
3G | Up to 42 mbs downlink; Up to 5.76 mbs uplink |
4G | Up to 100 mbs downlink; Up to 50 mbs uplink |
WIFI | Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, WIFI hotspot |
Bluetooth | Version4.0 |
GPS | A-GPS |
NFC | No |
USB | MicroUSB v2.0 |
Camera |
|
Primary | 13MP, up to 4128 x 3096-pixel pictures, HDR, autofocus, Geo-tagging, panorama camera with LED flash |
Video | 1080@30fps |
Secondary | 13MP, up to 4128 x 3096-pixel pictures, LED flash |
Battery |
|
Capacity | 2500mAh Li-Ion battery |
Stand-by | |
Talk time | |
Music play | |
Other Features |
|
Sensors | Accelerometer, Proximity, Fingerprint |
Messaging | SMS, MMS, Email, Push Mail, IM |
Browser | HTML5 |
Java | No |
– SNS integration – MP4/MPEG4/H.263/H.264 player – MP3/WAV/eAAC+/AC3/FLAC player – Document viewer – FM radio – Image viewer and editor – Voice memo/dial/command – Predictive text input – Preloaded apps – Gmail, Gtalk, Google Now, Youtube, Flash Share, Facebook, Palmchat |