Hii!! Natumai uko poa!! Leo napenda nikujulishe njia inayoweza kukusaidia kujua muda kamili ambao mtu uliyemtumia msg whatsapp ameisoma.Naomba ieleweke kuwa nachokizungumzia hapa sio zile alaama mbili za tiki ambazo hua zinakuonyesha kuwa ujumbe wako umeonwa au kufunguliwa,hapa nakuonyesha namna ambayo itakuonyesha saa,dakika,tarehe na mwaka ambao msg hiyo mhusika aliisoma.
Ni rahisi sana kuitumia mbinu hii na ikitokea bahati mbaya umesoma hujaelewa basi usisite kuniandikia kwenye comment hapo chini nami ntakusaidia.
Zifuatazo ni hatua au namna itakayoweza kukusaidia kufanya hiki tunachokijadili.
1.Fungua account yako ya whatsapp na kisha nenda kafungue msg ambayo unataka kujua muda ambao uliyemtumia ameisoma.
2.Ibonyeze kwa muda kama wa sekunde tatu bila kuachia msg hiyo unayotaka kujua au mpaka utakapooona kuna kama rangi ya bluu imetanda kwenye hiyo msg kisha achia.Kisha utaona kitu kama picha hii hapa chini
Baada ya hapo bonyeza kwenye alaama hiyo ipo kama i ambayo itakuwa juu kabisa kwenye hiyo msg uliyoibonyeza kama unavyoona hapo juu kwenye picha.Ukisha bonyeza kialama hicho basi chini ya hiyo msg itakuletea taarifa inayoonyesha muda ambao mhusika ameisoma msg na pia muda ambao mhusika alipokea msg hiyo kama inavyoonyesha hapa chini kwenye picha.
Ni hayo tu kwa leo,tafadhari usiache kushare na marafiki kama ujanja huu umeupenda!!
@NurFire,Spiro Spero!!
0 comments: