Friday, September 16, 2016

Namna ya kutuma msg moja whatsapp kwa watu wengi mara moja.

whatsapp tricks

Hii Rafiki!!  Natumai uko poa. Leo napenda nikujulishe njia rahisi ambayo inaweza kukusaidia kutuma ujumbe mmoja yaani msg moja kwa watu wengi kwa mara moja.Kwa kawaida imetuwia rahisi kutuma msg zetu kwa watu wengi kwa kutumia magroup ambayo tunakuwa nayo au kuyatengeza kwenye proggram zetu za whatsapp lakini changamoto inakuja pale unapohitaji kuwatumia watu fulani msg ya aina moja ambao hawako kwenye group moja.
    Chukulia mfano unataka kuwapa watu taarifa labda ya msiba ambao hawako kwenye group moja na kumtumia kila mtu mmoja mmoja ni shida kwahiyo hapa nataka nikuonyeshe namna itakayokusaidia kwenye changamoto kama hizo

             FUATA HATUA ZIFUATAZO 
 1.Fungua programu yako ya whatsapp,kisha angalia upande wa kulia wa akaunti yako ya whatsapp juu utaona vinukta vitatu.Bonyeza vinukta hivyo na yatatokea machaguo mbali mbali kama inavyoonyesha hapa chini kwenye picha.Kisha bonyeza new broadcast na itakuletea uwanja mwingine huku kukiwa na majina yote ya whatsapp yako.Baada ya hapo bonyeza [mark] kila jina ambalo unataka kuwatumia msg yako.
                                  Screenshot_2015-05-08-16-41-07
                                                          Baada ya hapo watumie msg ambayo unataka kuwatumia na itaenda kwa watu wote hao ambao umewaweka kwenye list hiyo kama ambavyo nimekuelekeza.Kitu muhimu unachotakiwa kukizingatia ni kwamba wote utakaokuwa unawatumia msg kwa mtindo huu wanatakiwa wawe na namba yako kwenye simu zao.

            Ni hayo tu kwa leo na nakutakia Wikendi njema.Usisahau kushare na marafiki!!
                                                
                                                    @NurFire Spiro Spero!!
 
banner
Previous Post
Next Post

0 comments: