
Hii!! Natumai uko poa!! Naamini katika ulimwengu huu wa teknolojia watu wengi wamekuwa wakifuatilia namna ambavyo teknolojia imekuwa ikiboresha vifaa vyake kila wakati.
Leo napenda nikujulishe mambo machache lakini muhimu kuhusu simu mpya kutoka kampuni kubwa kabisa ya Apple kwenye simu yao mpya ya Apple iPhone 7.Simu hii rasmi imeingia sokomi mwezi huu na kwa mujibu wa vyanzo vya habari vinasema kwamba watu wengi wamepanga foleni kwenye sehemu ambazo zinauza simu hizi kwaajili ya kununua,
Lakini kabla hujapata hamu ya kuwa mmoja ya watakaoendelea kupanga mstari kuinunua naoomba nikujulishe haya hapa ambayo ni muhimu kuhusu simu hii.
Kama ilivyokuwa kwenye iPhone 6 kulikua na matoleo mawili hali kadhalika nasasa kampuni hiyo imetoa simu yake hiyo mpya katika matoleo mawili yaani iPhone 7 na iPhone 7 plus hii ikamaanisha pia simu hizi zina sifa tofauti ingawa toleo lake ni moja.
Simu hii imetolewa ikiwa na rangi tofauti tofauti kama ambavyo unaweza kuona hapa chini na hivyo ni juu yako wewe kuchagua rangi unayoipenda.

Mambo mazuri kuhusu simu hii ni kama ifuatavyo..
1.Kioo chake [screen] kinang'aa vizuri sana.
2.Inafanya kazi kwa spidi kubwa
3.Ina Camera bora kabisa inayopiga picha za kiwango cha juu kwa ubora
4.Ina spika zilizopo mbele ya simu [front facing speakers]
Mapungufu kuhusu simu hii ya Apple iPhone 7
1.Haina camera mbili kama ilivyo kwenye iPhone 7 Plus
2.Haitumii Ear phone,Haina sehemu ya kuchomeka ear phone
3.Mambo mengi ambayo yanaonekana kuwa mapya kwenye simu hii sio kweli kuwa mapya kwani yalikuwepo kwenye matoleo mengine.
Kwa wataalamu wa simu wanasema kuwa simu hii namna ilivyotengenezwa imekuwa bora zaidi kwa wale wanaopenda kupiga picha,kutengeneza na kutazama video na pia kwa wale wanaopenda kucheza games kwenye simu zao.Hii ina maana kuwa simu hii kwenye maeneo hayo imaetengenezwa kwa ubora wa hali ya juu.
Mengine muhimu kuhusu simu hii tazama hapa chini.
Service Provider: Unlocked
Operating System as Tested: iOS 10
CPU: Apple A10
Dimensions: 5.44 by 2.64 by 0.28 inches
Form Factor: Candy Bar
Physical Keyboard: No
Weight: 4.87 oz
Screen Size: 4.7 inches
Screen Type: Retina
Screen Resolution: 1,334 by 750 pixels
Screen Pixels Per Inch: 326
Camera Resolution: 12MP Rear, 7MP Front-Facing |
Video Camera Resolution: 4K, 1080p |
Wireless Specification: 802.11n (2.4+5 GHz Dualband) |
Bluetooth Version: 4.2 |
GPS: Yes |
NFC: Yes |
Total Integrated Storage: 32 GB |
microSD Slot : No |
Phone Capability / Network: GSM, CDMA |
High-Speed Data: LTE |
Capacities Available: 32GB, 128GB, 256GB |
Colors Available: Jet Black, Black, Silver, Gold, Rose Gold |
0 comments: