NurFire says Hello!! Bila shaka mko poa.Leo napenda nikuonyeshe namna ya kuweza kutumia programu/Akaunti zaidi ya moja kwenye simu yako kutoka kwenye progamu ya aina moja.Nina maana hii,simu yako inaruhusu wewe kuhifadhi/kuinstal programu ya aina moja kuwa moja tu kwenye simu yako.Mfano unapokuwa na whatsap kwenye simu yako huwezi kuidownload whatsap hiyo hiyo ukaiweka tena kwenye simu na ukawa nazo mbili kwa wakat mmoja na kwenye simu hiyo hiyo moja.Lakini kutokana na matumizi kuna wakati unajikuta unatamani au ungehitaji kuwa na akaunti ya mprogrmu fulani zaidi ya mbili kwenye simu yako hiyohiyo moja.Mfano una whatsap moja ambayo umeisajili kwa no fulani na hivyo ungependa kuwa na whatsap nyingine kwenye simu hiyo hiyo moja na uisajili kwa no nyingine.Hapa nakueleza namna unavyoweza kufanikisha zoezi hilo na kuwa na programu zaidi ya moja kwenye simu yako hiyo hiyo moja.
FUATA HATUA ZIFUATAZO KUFANIKISHA HILO
1.Hakikisha simu yako ina nafasi ya mb karibu 500.
2.Hakikisha toleo la simu yako ni version ya android 4 na kuendelea.
3Kama hayo hapo juu unayo endelea kwa kudownload programu iitwayo Parallel space kwa kubonyeza kwenye anuani moja wapo kati ya hizi mbili hapa chini
1.parallel-spacemulti-accounts-2-1-4589-apkplz.com.apk - 3.4 MB
2.parallel-spacemulti-accounts-2-1-4589-apkplz.com.apk - 3.4 MB
3.Baada ya kudownload programu hiyo kisha ihifadhi/instal kwenye simu yako.
4.Ikishamaliza kuinstall bonyeza chaguo open ili kuweza kuifungua na ikishafunguka utaona nembo yenye alama ya kujumlisha bonyeza hapo.
5.Baada ya kubonyeza nembo ya alama ya kujumlisha kisha utaziona programu zako ulizozihifadhi kwenye simu yako kama inavyoonyesha hapa chini.baada ya hapo bonyeza alama ya kunyumlisha iliyopo chini ya programu hizo ili uweze kuongeza programu unayoitaka.kisha utaongeza hiyo programu na utakuwa umeshamaliza na utaweza kuwa na progrmu mbili za aina moja kwenye simu yako.
KUMBUKA;ili uweze kufungua progrmu uliyoiongeza itakubidi ufungue kwanza parallel space program na ndani yake ndiyo utaikuta ile programu uliyoongeza Ahsante kwa leo.Kama hujaelewa au una tatizo lolote tafadhari niandikie kwenye maoni hapo chini
0 comments: